MWANANCHI Maofisa 12 wa LBL Mbaroni, Kampeni ‘Sitapeliki’ Yazinduliwa Alhamisi, Februari 20, 2025 Na Waandishi Wetu Morogoro/Arusha. Wakati Jeshi la Polisi likiwashikilia watu 12 katika mikoa ya Mbeya na Morogoro kwa tuhuma za kuendesha biashara ya fedha mtandaoni bila kibali cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Serikali imezindua kampeni maalumu ya kudhibiti vitendo vya kitapeli na ulaghai mtandaoni. Kampeni hiyo, inayojulikana kama Sitapeliki , inalenga kutoa elimu kwa umma kuhusu udanganyifu wa kifedha na njia za kujikinga na matapeli wa mtandaoni. Pia, inahimiza wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya majaribio ya ulaghai yanayofanywa na watu wachache kwa lengo la kujinufaisha. BoT imeonya kuwa wale wanaoendesha michezo ya fedha mtandaoni bila leseni watachukuliwa hatua kali za kisheria. Kampeni hiyo imezinduliwa leo, Alhamisi Februari 20, 2025, na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa, wakati wa kikao kazi kati ya Serikali na wadau wa sekta ya mawasiliano kili...